NAFASI YA KAZI -NAFASI MBILI
Grace
College ni chuo kilicho chini ya Kanisa la Neema Tanzania chenye usajili wa
Mamlaka ya mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA). Chuo kipo Mtaa wa Forest karibu na
Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Mbeya. Grace College tunatoa Kozi zifuatazo
Uhazili(Secretarial) Mwaka Mmoja,
Hoteli na Utalii (Hotel Management and Tourism) Miezi Sita, Utalii na Uongozi(Tourism and Management) Miezi Sita, Kozi Fupi za Kompyuta
(Computer Courses) Miezi Miwili na
Kozi za Lugha ( English and French Courses) Miezi Mitatu.
Tunayofuraha kuwatangazia nafasi ya kazi ya ualimu wa hoteli kwa wanafunzi wa ngazi ya Cheti,
SIFA ZA MWOMBAJI
1. Awe ana stashahada ya hoteli kutoka chuo chochote
2. Awe na sifa za kufundisha ama zifanano
3. Awe anajua kiingereza kwa ufasaha
4. Awe na taaluma ya kutumia kompyuta
5. Awe na uwezo wa kufundisha kozi zote za hoteli
Barua ya maombi, CV na Nakala ya vyeti vyote vitumwe kwa Mkuu wa chuo kupitia barua pepe (Email) gracecollege2001@gmail.com